KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA MAOMBI KWA MUHULA WA MWEZI WA TATU 2024/2025

Ofisi ya Mkuu wa chuo TRACDI inapenda kuwaarifu wazazi ,walezi na wanafunzi kuwa Baraza la Elimu ya Ufundi na mafunzo ya ufundi Stadi NACTVET limefungua rasmi dirisha la maombi ya kujiunga na  masomo kwa ngazi ya Certificate na Diploma kwa muhula utakaonza mwezi wa Tatu 2024.

 Mkuu wa chuo anapenda kuwakumbusha kuwa chuo kinatoa  mafunzo katika kozi za Kilimo,Mifugo na Maendeleo ya Jamii kwa ngazi ya Certificate na Diploma.

kozi  Kwa Muhula wa mwezi wa Tisa chuo kinadahili katika kozi za Maendeleo ya Jamii pamoja na kozi ya Kilimo, kozi ya Mifugo inatolewa kwa muhula mmoja tu mwaka ambao ni muhula wa mwezi wa Tisa.

 Pia chuo kinatoa Mafunzo ya Kilimo na Ufugaji kwa ngazi ya VETA kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha nne kwa ufaulu usiopungua masomo mawili.

 Unaweza kufanya mamombi kwa Kudownload Fomu kwa kubonyeza Link ya Application kwenye website ya chuo au kupitia Online Application.

 Masomo yataanza mwezi wa Tatu tarehe 25

Chuo kitakuwa na mafunzo maalumu kwa wanafunzi kama vile Kuendesha Trekta,mafunzo ya namna bora ya ufugaji wa kisasa pamoja mafunzo ya ujasiliamali.

 Hivyo wanafunzi wote watakaoomba nafasi wanashauriwa kuripoti mapema chuoni kuanzia tarehe 10/03/2024

 Maombi yanapokelewa kuanzia sasa,amombi yanafanyika kupitia Website ya chuo www.tracdi.ac.tz/apply online au fika chuoni   moja kwa moja eneo la Nzuguni.

  Nyote mnakaribishwa